Twange: Mradi wa kuzalisha Umeme wa Jua Kishapu wafikia asilimia 63.3

📌Asema awamu ya kwanza utazalisha Megawati 50 na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange amesema Mradi wa uzalishaji umeme unaotokana na jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63.3 kukamilika ambapo amesema awamu ya kwanza ya Mradi huo utazalisha Megawati 50 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.

Twange ameyasema hayo leo Juni 8 mwaka 2025 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo ambao unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 118 kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikitarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 204.

‘’Kwanza tunamshukuru Rais kwa kutupatia fedha kwa awamu zote, kama mnavyoona kazi inaendelea na Mradi unatarajia kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa mwishoni mwa mwezi wa kumi kwa ajili ya kuwasambazia umeme wananchi, lakini pia tuko katika hatua za mwisho za manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayetekeleza Mradi kwa awamu ya pili ambayo itazalisha megati 100’’ alisisitiza Twange.

Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa TANESCO inafanya jitihada za makusudi za kuhakikisha Mradi unakamilika kwa wakati ili kuendana na ongezeko la mahitaji ya watu na shughuli za uwekezaji ambazo zinategemea nishati ya umeme kujiendesha.

Naye Meneja wa Mradi huo Mhandisi Emmanuel Andarson amesema awali Mradi huo ulipaswa kukamilika mwezi February mwaka huu lakini Mkandarasi aliongezewa muda baada kukabiliwa na baadhi ya changamoto ambapo ameahidi kukamilisha Mradi huo kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba .

Mradi wa uzalishaji wa umeme unaotokana na nguvu ya jua wa Kishapu uliopo katika Kijiji cha Ngunga Mkoani Shinyanga ulianza utekelezaji wake Desemba 8 mwaka 2023 na unatarajia kukamilika rasmi Oktoba 29 2025 ambapo unagharimu jumla ya shilingi bililioni 323 kwa awamu zote mbili ukitarajia kuzalisha megawati 150 za umeme.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this