TMA yatabiri kipupwe chenye baridi kali, upepo mkali na mvua za nje ya Msimu 2025

Na Tatu Mohamed

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri rasmi wa hali ya hewa kwa msimu wa Kipupwe unaotarajiwa kuanzia Juni hadi Agosti 2025, ikibainisha hali ya baridi kali, upepo mkali na uwezekano wa mvua za nje ya msimu katika maeneo kadhaa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 22, 2025 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chan’ga, ambaye amesisitiza umuhimu wa wananchi na wadau wa sekta mbalimbali kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa.

Kwa mujibu wa Dkt. Chan’ga, msimu wa Kipupwe 2025 utatawaliwa na hali ya baridi ya wastani hadi kali, hasa katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Singida na magharibi mwa Dodoma. Julai umetajwa kuwa mwezi wenye baridi kali zaidi, ambapo baadhi ya maeneo yenye miinuko yanatarajiwa kushuka chini ya nyuzi joto 6°C, hasa katika nyanda za juu kusini-magharibi mwa Tanzania.

TMA pia imetabiri vipindi vya upepo mkali kutoka kusini (upepo wa kusi), vitakavyotawala maeneo mengi ya nchi, hasa katika ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.

“Upepo huu unatarajiwa kuongezeka zaidi katika miezi ya Juni na Julai, hali inayoweza kuchochea vumbi na kuongeza hatari ya matatizo ya kiafya hasa kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa upumuaji,” amesema Dkt Chang’a.

Amesema pamoja na ukavu wa kawaida wa Kipupwe, baadhi ya maeneo yanatarajiwa kupata mvua za nje ya msimu.

“Mikoa ya kanda ya Ziwa Victoria ikiwemo Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara, pamoja na ukanda wa pwani na visiwa vya Unguja na Pemba, vinatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua visivyokuwa vya kawaida kwa msimu huu.

“Athari zinazotarajiwa kutokana na hali hiyo ya hewa ni pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya kuambukiza kama homa ya mapafu, magonjwa ya mifugo, na matatizo yanayohusiana na vumbi,” amesema.

Ameongeza kuwa, ukame unaweza kusababisha upungufu wa maji na malisho kwa mifugo katika baadhi ya maeneo, hasa yale yanayokumbwa na upepo mkali na baridi kali.

Ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuvaa mavazi ya joto, kujikinga dhidi ya vumbi na kuwahudumia mifugo yao kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Wakulima pia wamehimizwa kutumia maeneo yenye unyevunyevu kwa kilimo cha mazao ya muda mfupi kama mboga mboga, ili kuendana na hali ya hewa inayotarajiwa.

Watumiaji wa shughuli za baharini nao wametakiwa kuwa makini na kufuatilia utabiri wa kila siku kuhusu hali ya upepo na bahari kwa ajili ya usalama wao.

Vipindi vya upepo mkali vinaweza kuhatarisha shughuli za uvuvi na usafiri wa baharini.

TMA imesisitiza kuwa itaendelea kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Wananchi na wadau wanahimizwa kufuatilia utabiri wa saa 24, siku 10 na mwezi kupitia tovuti rasmi ya TMA www.tma.go.tz pamoja na akaunti zake kwenye mitandao ya kijamii kwa tahadhari na miongozo muhimu.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...