Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O dhidi ya mpinzani wake Stanley Eribo kutoka Nigeria, baada ya kumaliza pambano katika raundi mbili.

Pambano hilo limemalizika usiku huu katika ukumbi wa Warehouse Masaki, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo amesema imekuwa rahisi kwake kumshinda mpinzani wake kutokana na mazoezi anayofanya bila kujali ana mchezo au hana.

Amesema ubora wake haushuki hata akikaa muda mrefu bila kucheza kwa kuwa ameweka heshima katika mazoezi na anaamini ndiyo mhimili wa kazi yake.

Katika pambano lingine Mtanzania Hamadi Furahisha ameibuka mshindi kwa pointi dhidi ya Mmalawi Hanock Phiri katika pambano la raundi 10, huku Hassan Ndonga akimchapa Ismail Boyka.

spot_img

Latest articles

“MADEREVA TANESCO KUWENI CHACHU UTOAJI HUDUMA BORA”

📌Watakiwa kutunza vyombo vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa huduma 📌TANESCO yanunua vyombo vya usafiri...

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...

CRDB yazindua msimu wa nne wa Zogo Mchongo, yasisitiza elimu ya fedha na matumizi ya teknolojia kukuza uchumi

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB imezindua rasmi msimu wa nne wa kipindi cha Zogo...

More like this