Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limemkamata Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Daines Faustine (33) kwa tuhuma za kukutwa akiendesha gari akiwa amelewa kupita kiasi, hali iliyosababisha kushindwa kulidhibiti gari hilo na kugonga taa za barabarani katika eneo la Bigwa Manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama, tukio hilo limetokea Mei 17, 2025, ambapo Faustine ambaye ni mkazi wa Morogoro, alikuwa akiendesha gari aina ya Nissan Juke alipokamatwa. Uchunguzi wa kitabibu umebaini alikuwa na kiwango cha pombe mwilini cha 305.9.
Amesema katika tukio lingine, dereva Bakari Omari (47), mkazi wa Kondoa mkoani Dodoma, amekamatwa akiendesha gari mali ya Kampuni ya Machame Investment judoka Dar es Salaam kwenda Dodoma bila kuwa na leseni.
Kamanda Mkama amesema uchunguzi umebaini kuwa dereva huyo alikuwa tayari amepigwa marufuku kuendesha magari tangu Mei 5, 2025, kufuatia mwenendo wake wa kuendesha mwendo hatarishi barabarani. Hata hivyo, alikaidi agizo hilo na kuendelea kuendesha gari kwa kificho hadi aliponaswa na vyombo vya usalama Mei 18, mwaka huu 2025.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linaendelea na operesheni maalum ya kudhibiti usalama katika barabara zote mkoani humo. Lengo kuu la operesheni hii ni kulinda na kuokoa maisha ya watumiaji wote wa barabara pamoja na vyombo vya moto kwa kuhakikisha sherry na kanuni za usa lama barabarani zinazingatiwa,” imesema taarifa hiyo.