Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei ametajwa kuwa kinara wa kuzungumzia mahitaji ya wananchi kwa kuwa miongoni mwa wabunge vinara wa kusema, kuchangia au kuhoji katika kila kikao cha bunge akiwa amechangia mara 49 na kuuliza maswali 110 kwa mujibu wa tovuti ya Bunge la Tanzania.

Aidha ni aina ya wabunge wanaoonekana katika majimbo yao wakifanya mikutano ya wananchi kutoa mrejesho, kusikiliza na kutatua kero pamoja na ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo.



