GF Automobile, NaCoNGO zasaini makubaliano ya kimkakati kusaidia vijana

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya GF Trucks kupitia kampuni ya GF Automobile imeingia makubaliano na Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NaCoNGO ), yakilenga kunufaisha pande zote mbili katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya GF Trucks ,Mujtaba Karmali amesema wao kama wauzaji wa magari na mitambo wameoana kuna haja ya kuingia makubaliano hayo ya kimkakati ambapo pia watatoa elimu, kuwajengea uwezo na uelewa katika maeneo tofauti.

Aidha Karmali amesema tayari wao wameanza mpango wa kutoa mafunzo kazi kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali mfano , VETA na DIT ili kuwajengea uwezo wa kuweza kufanya kazi na kupata uzoefu kazini.

” Makubaliano haya yatarahisisha kuwafikia makundi ya vijana nchi nzima na kuungana na serikali katika mpango wa kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri kwa kupita katika vyuo mbalimbali,” ameeleza Karmali.

Nae Mwenyekiti wa NaCoNGO , Jasper Makala ameishukuru kampuni ya GF Trucks kwa kuonyesha njia kwa makampuni ya Kitanzania kuchangia maendeleo ya jamii kupitia mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.

Amesisitiza kuwa ushirikiano na makampuni binafsi ya ndani ya nchi ni mbinu mojawapo ya kupunguza utegemezi toka nje ya nchi kuelekea katika uendelevu wa mashirika.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this