Kapinga: Ni maono ya Dkt. Samia wananchi wapate umeme

📌 Asema wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia madarakani Vijiji 4000 havikuwa na umeme

📌 Aitaka TANESCO na REA kuendelea kutoa elimu ya kuunganisha umeme

📌 Nishati ya umeme yauongezea ufanisi Zahanati ya Mang’oto

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona wananchi wote wanapata huduma ya umeme.

Kapinga ameyasema hayo Machi 17, 2025 katika Kijiji cha Mang’oto Wilaya ya Makete mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

“Mheshimiwa Rais legacy yake na maono yake ni Tanzania nzima mijini, vijijini na vitongojini kupata umeme, ndio maana mnamuona anahangaika kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya umeme kwenye Vitongoji,” amesema Kapinga.

Ameongeza kuwa mwaka 2020 Serikali iliahidi kuvifikishia umeme vijiji vyote 12,318 ifikapo Desemba 2025 na wakati Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani takribani Vijiji 4000 havikuwa vimefikiwa na huduma ya umeme.

Katika hatua nyingine, Kapinga amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuendelea kutoa ushirikiano kwa wananchi pamoja na utoaji wa elimu wa jinsi ya kufanya maombi ya kuunganisha umeme.

Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa kutumia namba 180 ambayo haina malipo kwa mteja Mhe. Kapinga amesisitiza kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha umeme wa uhakika na unaotabirika unawafikia wananchi wote ili waweze kunufaika kwa shughuli za kiuchumi.

Kufika kwa umeme katika Kijiji cha Mang’oto kumewanufaisha wananchi ambapo wamefungua shughuli za kiuchumi ikiwemo mashine za kusaga nafaka lakini pia kuweza kurahisisha huduma katika Zahanati ya Mang’oto ambayo hapo awali ilikuwa ikitumia umeme wa jua.

Kutokana na hilo wananchi wameipongeza Serikali kwa utekelezaji wa miradi ya umeme Vijijini kwani wameweza kuinua vipato vyao ikiwemo kufungua biashara kama za kuchomelea na kuboresha huduma za afya.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

More like this

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...