Mkenda: Tutaendelea kuimarisha ushirikiano sekta ya nguo na mavazi

Na Tatu Mohamed

SERIKALI imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yao, viwanda na wabunifu ili kufanikisha maendeleo katika sekta ya nguo na mavazi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, katika Kongamano la kujadili maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta hiyo lililoandaliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kuelekea maadhimisho ya miaka 30.

Amesema asilimia kubwa ya wanaojihusisha katika sekta hiyo hawana kiwango kikubwa cha elimu lakini wanao ujuzi na ubunifu mzuri katika kutengeneza bidhaa zinazovutia.

“Tunawahitaji sana katika kuimarisha ujuzi tunaoutaka, kwani itawasaidia wanafunzi wetu kujifunza kwa vitendo kupitia nyinyi. Naipongeza VETA kwa kuandaa kongamano hili, na endeleeni kujenga mahusiano mazuri na wadau hawa muhimu.

“Ndoto ya serikali na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha tunazalisha bidhaa zenye ubora kwa wingi ili tuuze ndani na nje ya nchi,” amesema Profesa Mkenda.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore amesema lengo la kongamano hilo ni kukutana na kujadili namna VETA inaweza kushirikiana na wadau hao ili kuendeleza sekta hiyo.

“Mada mbalimbali zimewasilishwa katika kongamano hili na katika kujadiliana tumeona wadau ni wengi na soko ni kubwa, hivyo tunatakiwa kulitumia ili kuzalisha bidhaa za kutosha,” amesema.

Mbunifu wa Mavazi, Miriam Ekilwa amesema: “Tunafurahi hatua ya serikali kutambua umuhimu wetu. Ni matarajio yetu ushirikiano huu unafanyika kwa vitendo ili kuikuza sekta hii muhimu,”.

spot_img

Latest articles

Tamasha la Singeli Agosti 2 wasanii kutoa burudani ya Kimataifa

Na Winfrida Mtoi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa,...

Maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum UVCCM yamekamilika

Pichani ni Viongozi wa sekretarieti ya Umoja wa Vijana CCM wakikabidhi vifaa mbalimbali wezeshi...

INEC: Hakuna atakayeachwa nyuma kwenye Uchaguzi Mkuu 2025

Na Tatu Mohamed TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema imeweka mazingira wezeshi...

Serikali yawataka wakuu taasisi za umma kutengeneza mazingira rafiki ya kazi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewataka wakuu wa taasisi za umma kutengeneza mazingira rafiki ya...

More like this