DAWASA yawatangazia fursa wenyeviti wa mitaa

Na Tatu Mohamed

KAIMU Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire ametangaza fursa lukuki kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Kigamboni zitakazotokana na ushirikiano bora uliitengenezwa baina yao na Mamlaka hiyo.

Mhandisi Bwire amebainisha fursa hizo katika kikao kazi na wenyeviti hao kilicholenga kuboresha mahusiano na kujenga ukaribu baina ya Serikali za Mitaa na DAWASA.

“Ukaribu huu unakuja na fursa nyingi ndugu wenyeviti ambazo zitanufaisha pande zote mbili , Serikali pamoja na wenyeviti kama mtu mmoja mmoja, kuanzia saa wwenyekiti atakaetusaidia kuhamasisha maunganisho na kutuletea wateja atapata kiasi cha Shilingi 10,000 kwa kila mteja mmoja anaemleta,” amesema Mhandisi Bwire.

Bwire amesema sio hivyo tu lakini hata kwa wale ambao watasaidia kufichua wahujumu kwa Mamlaka mfano wezi wa maji hawataacha hivi hivi bali nao watanufaika kwa uzalendo watakaouonyesha.

“Ndugu zangu wenyeviti kwa kila mmoja wenu atakae saidia kubaini mwizi wa maji na tukamkamata na kumpiga faini basi Mwenyekiti uliesaidia kubaini hilo utapata asilimia 30 ya fedha zitakazolipwa kama faini,” amesema Mhandisi Bwire

Amesema motisha hii kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa itakua chachu ya wao kushirikiana na Mamlaka zaidi katika shughuli za kila siku kuwapatia huduma ya maji wananchi.

Ameongeza kuwa, hawataishia hapo tu bali watatoa motisha kwa kila Mwenyekiti atakaesaidia kushawishi mteja aliesitishiwa huduma Kulipa deni lake na kurudi kutumia huduma za DAWASA.

Hatua hii imepokelewa vyema na wenyeviti waliohudhuria kikao kazi hicho huku wakiahidi kufanya kazi bega kwa bega na DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora ya Majisafi wakati wote.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...