Ndejembi amsimamisha kazi Afisa ardhi Handeni

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga kumsimamisha kazi na kumchukulia hatua za kinidhamu, Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mji Handeni kwa kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi kwenye Halmashauri hiyo.

Ndejembi ametoa agizo hilo Januari 20, 2025 alipofanya ziara katika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga ambapo alitembelea eneo la Kwanjugo Kitalu A ambalo wananchi wake wamekua wakilalamika kwa muda mrefu kuchukuliwa maeneo yao bila kulipwa fidia.

“Hapa kiasili pana historia yake, palikua pana umiliki wa wenyewe sasa haiwezekani watu hawa kuonewa, na migogoro yote hii ni kwa sababu hatusikilizi wananchi wetu, sasa ninamuelekeza Katibu Mkuu kumsimamisha mara moja Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri na haraka sana aletwe mtu mwingine atakayeweza kutatua migogoro ya ardhi Handeni.

“Lakini pia ninaelekeza kuundwa kwa Timu ya uchunguzi itakayokua chini ya Kamishna wa Ardhi, ije hapa Handeni ndani ya wiki moja ili ichunguze umiliki wa viwanja vya sasa ni akina nani, na kama ni watumishi wa ardhi tuchukue hatua kali. Kwa sababu hatuwezi kuruhusu watumishi wa ardhi kunyang’anya ardhi ya wananchi,” amesema Ndejembi.

spot_img

Latest articles

Kwa nini ninatamani Polepole anyamaze milele?

JUMATATU wiki hii Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipitisha majina ya wanachama wake watakaopigiwa kura...

Mnyama Simba anaachia tu vifaa vyake

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba leo Julai 30, 2025, imemtambulisha Alassane Kante raia wa...

Chalamila awaalika wakazi wa Dar kujitokeza kwa wingi uzinduzi wa Kituo cha biashara cha EACLC

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaalika Watanzania na...

Ajali ya moto yaua watoto yatima watano

Na Mwandishi Wetu Watoto watano waliokuwa wanalelewa katika kituo cha watoto yatima cha Igambilo Manispaa...

More like this