Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ashiriki ibada ya kumuaga mama mzazi wa Waziri Mkenda

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango leo Februari 06, 2025, wameungana na viongozi na wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuaga marehemu Sekunda Massawe ambaye ni Mama mzazi wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Pius X – Tarakea mkoani Kilimanjaro.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Mpango amesema Serikali, inashukuru kwa maisha ya mama Sekunda aliyemzaa na kumlea Prof. Mkenda, ambaye amekuwa Mtendaji na Kiongozi mahiri katika utumishi wa umma, tangu alipokuwa anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam na katika nafasi mbalimbali alizoshika Serikalini.

Amesema Taifa linaendelea kufaidi matunda ya malezi bora na uchapakazi, ambayo mama Sekunda aliwapatia watoto wake.

Ametoa rai kwa wazazi na walezi kufanya kila jitihada kusomesha watoto, kuwafundisha maadili mema, kushika dini yao kiadilifu, na kufanya kazi kwa bidii kwa faida yao wenyewe, familia na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, kila mmoja anapaswa kujitahidi kuishi vema na binadamu wenzake na kufanya kazi kwa bidii katika nafasi mbalimbali ili kutoa mchango mzuri kwa familia na Taifa, na kuacha historia nzuri na mifano bora ya kuigwa na jamii. Ameongeza kwamba ni muhimu kujiandaa kumrudia Muumba maana hakuna ajuaye siku wala saa.

Ibada ya kumuaga marehemu Sekunda Massawe imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi Mhashamu Ludovick Minde na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wabunge, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Viongozi wa Dini pamoja na wananchi mbalimbali.

spot_img

Latest articles

Kwa nini ninatamani Polepole anyamaze milele?

JUMATATU wiki hii Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipitisha majina ya wanachama wake watakaopigiwa kura...

Mnyama Simba anaachia tu vifaa vyake

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba leo Julai 30, 2025, imemtambulisha Alassane Kante raia wa...

Chalamila awaalika wakazi wa Dar kujitokeza kwa wingi uzinduzi wa Kituo cha biashara cha EACLC

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaalika Watanzania na...

Ajali ya moto yaua watoto yatima watano

Na Mwandishi Wetu Watoto watano waliokuwa wanalelewa katika kituo cha watoto yatima cha Igambilo Manispaa...

More like this

Kwa nini ninatamani Polepole anyamaze milele?

JUMATATU wiki hii Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipitisha majina ya wanachama wake watakaopigiwa kura...

Mnyama Simba anaachia tu vifaa vyake

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba leo Julai 30, 2025, imemtambulisha Alassane Kante raia wa...

Chalamila awaalika wakazi wa Dar kujitokeza kwa wingi uzinduzi wa Kituo cha biashara cha EACLC

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaalika Watanzania na...