MACHIFU watano wametekwa nyara siku ya Jumatatu na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabaab katika Kaunti ya Mandera nchini Kenya.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki John Otieno amesema machifu hao watano walikuwa wakielekea Elwak walipotekwa nyara kati ya Bamba Owla na Ires Suki.
Ripoti inaonyesha wasimamizi wa eneo hilo walipaswa kufanya mkutano kabla ya ziara ya Rais William Ruto katika eneo hilo.Kwa sasa Rais William Ruto yuko kweney ziara ya wiki moja katika eneo la Kaskazini Mashariki, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kushirikiana na jamii za eneo hilo na kushughulikia vipaumbele vya maendeleo ya kikanda.
Chanzo: BBC