Na Mwandishi Wetu
Mnyama Simba amefanikiwa kuondoka na alama moja dhidi ya Orlando Pirates baada ya timu hizi kutoka sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza wa Kundi C wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uliopigwa leo Jumapili, Novemba 29,2026, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Simba iliongoza kipindi cha kwanza, ikienda mapumziko kifua mbele ikiongoza mabao 2-0. Mabao hayo yalifungwa na Libasse Gueye (dakika ya 10) na Anthony Mligo (dakika ya 42).
Hata hivyo furaha ya wanasimba iliisha baada ya Orlando Pirates kusawazisha mabao yote mawili kupitia kwa Tshepang Moremi (dakika ya 53) na Simphiwe Selepe (dakika ya 63).


