Mchezaji auawa na majambazi nchini Ghana

MCHEZAJI wa soka nchini Ghana, Dominic Frimpong, ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya jana Jumapili usiku  na majambazi wenye silaha kushambulia basi la timu yake ya Berekum Chelsea.

Tukio hilo lilitokea katika barabara ya Goaso–Bibiani wakati timu ikirejea nyumbani baada mchezo wa ya Ligi Kuu ya Ghana dhidi ya Samartex katika mji wa Samreboi kusini mwa Ghana.

 Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika klabu hiyo, majambazi hao walifunga barabara na kuanza kulishambulia basi lilikuwa limebeba viongozi na wachezajiwakati dereva akijaribu kurudi nyuma.

 Jeshi la Polisi nchini humo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Frimpong alifariki  wakati akipatiwa matibabu hospitalini kutokana na majeraha ya risasi.

 Chama cha Soka nchini Ghana(GFA) katika taarifa yake iliyotoa leo Jumatatu Aprili 13,2026, kimesema kimepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa, huku kikimueleza  mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kuwa mwenye kipaji na mapenzi ya mchezo huo.

 Timu hiyo imekumbwa na mkasa huo wakati  ilipokuwa ikirejea kutoka  kwenye mchezo wa Ligi  Kuu ya Ghana dhidi ya Samaetex huko  Samreboi. Umbali wa kilomita 270 kutoka Berekum.

spot_img

Latest articles

Wakurugenzi Media Brains waapishwa kuwa Majaji tuzo za EJAT

Na Mwandishi Wetu WAKURUGENZI wa Kampuni ya Media Brains wameapishwa wameteuliwa na Baraza la Habari...

CRDB yaandika historia, yapata faida ya Trilioni 1

Na Mwandishi wetu BENKI ya CRDB imepata faida ya Sh trilioni moja kabla ya...

Taliss IST yaendelea kutawala Mashindano ya Taifa ya Kuogelea, nahodha afichua siri

Na Winfrida Mtoi KLABU ya Taliss IST imezidi kujikita kileleni mwa mchezo wa kuogelea nchini...

Serikali yazindua shindano la ‘Vijana Uchumi Challenge’ kuibua ubunifu wa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka,...

More like this