Wakurugenzi Media Brains waapishwa kuwa Majaji tuzo za EJAT

Na Mwandishi Wetu

WAKURUGENZI wa Kampuni ya Media Brains wameapishwa wameteuliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuwa miongoni mwa majaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania 2026 (EJAT).

Walioteuliwa ni Jesse Kwayu, Absalom Kibanda na Neville Meena, ni miongoni mwa majaji 12 wa tuzo hizo waliapishwa wameapishwa leo Aprili 13, 2026 jijini Dar es Salaam na Wakili Ally Kileo,

Wengine wanaunda jopo hilo la majaji ni Joyce Shebe, Beatrice Bandawe, Rashid Kejo, Dk. Egbert Mkoko, Hassan Mhelela, Mwanzo Millinga, Sauli Gilliard, Shifaa Said Hassan na Aisha Dachi.

Akizungumzia uteuzi huo, Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura amesema mfumo huo mpya wa majaji ni mabadiliko makubwa kutoka kwenye tathmini za kizamani zilizokuwa zikizingatia zaidi ubora wa uandishi na uhariri pekee. 

Sungura amebainisha kuwa wakati mchujo wa awali wataendelea kuzingatia misingi mikuu ya uandishi wa habari ikiwamo usawa, uwiano, uwazi, na usahihi hatua ya fainali sasa itahitaji uthibitisho wa matokeo ya kazi hiyo katika jamii.

“Kwa sasa tunaenda na mfumo mpya “Uhakiki wa nyanjani” (Field verification) unaolenga kuimarisha uaminifu wa vyombo vya habari kwa jamii,” amesema Sungura.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this