Taliss IST yaendelea kutawala Mashindano ya Taifa ya Kuogelea, nahodha afichua siri

Na Winfrida Mtoi

KLABU ya Taliss IST imezidi kujikita kileleni mwa mchezo wa kuogelea nchini baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Taifa ya Klabu kwa mara ya tisa mfululizo.

​Katika mashindano hayo ya 18 tangu kuanzishwa kwake, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Aprili 10 na kutamatika jana, Taliss imedhihirisha ukongwe wake kwa kujikusanyia jumla ya pointi 448.5.

​Nafasi ya pili imenyakuliwa na klabu ya Dar Swim Club iliyopata alama 320.5, huku Mwanza Swimming Club ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 133. Mashindano hayo yalikuwa na ushindani mkali yakishirikisha waogeleaji 200 kutoka klabu 16, zikiwemo klabu mwalikwa kutoka nchi za Kenya na Zambia.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kombe, Nahodha wa Taliss IST, Romeo-Mihaly Mwaipasi, amesema siri kubwa ya mafanikio yao ni nidhamu ya hali ya juu na maandalizi ya kina.

​Romeo alibainisha kuwa ushindi wa mwaka huu una maana kubwa kwao kutokana na changamoto walizopitia, ikiwemo hali ya hewa ya mvua na kupungua kwa idadi ya wachezaji wao tegemeo.

​”Tumefurahi sana kutwaa ubingwa huu kwa mara ya tisa. Mwaka huu tulikuwa na changamoto ya idadi ya wachezaji kwani wenzetu wengi wamejiunga na masomo ya chuo kikuu. Hata hivyo, kocha alituhimiza kupambana, na jitihada binafsi za kila muogeleaji pamoja na bidii katika mazoezi ya kila siku ndivyo vimetubeba,” alisema Romeo.

Romeo ameweka wazi kuwa hatashiriki mashindano ya CANA Zone III yatakayofanyika Uganda mwaka huu kutokana na ratiba ya mitihani. Hata hivyo, ametoa rai kuwa Tanzania itafanya vizuri kutokana na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na waogeleaji katika michuano hii ya Taifa.

Naye mchezaji wa klabu ya Lake Victoria, Richard Makala amesema  kufanya vizuri katika mashindano ya Taifa, anaamini akichaguliwa kwenda kuiwakilisha nchi China, atafanya vizuri pia. “Nadhani nimefanya vizuri sana katika kundi letu la waogeleaji wa umri wa miaka 13-14, nilichohitaji ni kupunguza muda wangu zaidi,”  

​Kuelekea mashindano ya kimataifa, Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Mchezo wa Kuogelea Tanzania (TSA), Amina Mfaume, amesema mchakato wa kuchagua wachezaji watakaoiwakilisha nchi.

​Miongoni mwa mashindano yanayokusudiwa ni pamoja na ya Dunia ya World Aquatics Short Course Championship 2026, ambapo TSA inalenga kupeleka kikosi imara kitakachopeperusha vyema bendera ya Taifa.

spot_img

Latest articles

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...

CRDB yazindua msimu wa nne wa Zogo Mchongo, yasisitiza elimu ya fedha na matumizi ya teknolojia kukuza uchumi

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB imezindua rasmi msimu wa nne wa kipindi cha Zogo...

WAZIRI NDEJEMBI ATOA ONYO KWA MKANDARASI ANAYETEKELEZA MRADI WA SONGEA–TUNDURU–MASASI

📌 Asema ucheleweshaji wa mradi hauendani na matarajio ya Serikali na wananchi. 📌 Amuagiza mkandarasi...

Taasisi za umma zatakiwa kuachana na utendaji wa mazoea ili kufanikisha Dira 2050

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imezitaka Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kuachana...

More like this

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...

CRDB yazindua msimu wa nne wa Zogo Mchongo, yasisitiza elimu ya fedha na matumizi ya teknolojia kukuza uchumi

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB imezindua rasmi msimu wa nne wa kipindi cha Zogo...

WAZIRI NDEJEMBI ATOA ONYO KWA MKANDARASI ANAYETEKELEZA MRADI WA SONGEA–TUNDURU–MASASI

📌 Asema ucheleweshaji wa mradi hauendani na matarajio ya Serikali na wananchi. 📌 Amuagiza mkandarasi...