CRDB yaandika historia, yapata faida ya Trilioni 1

Na Mwandishi wetu

BENKI ya CRDB imepata faida ya Sh trilioni moja kabla ya kodi katika Kipindi cha mwaka 2025 ikiwa ni mara ya kwanza kuandika historia hiyo.

Akizungumza wakati wa sherehe za utoaji tuzo za CEO AWARDS zilizofanyika katika Ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt Abdulmajid Nsekela, amesema hatua hiyo imeifanya benki izidi kutambuliwa ndani na nje ya nchi na kutunukiwa tuzo nyingi kama vile kutambuliwa kuwa benki bora Tanzania, benki bora kwa wateja wadogo na wa Kati ambazo zinaenda sambamba na ubora wa wafanyakazi walionao.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Dkt Ally Laay, amesema anajivunia utendaji uliotukuka wa Dkt Nsekela kutokana na mafanikio iliyopata benki hiyo kwa kipindi kifupi tangu achukue nafasi hiyo.

Amesema wakati Dkt Nsekela anachukua nafasi ya CEO hisa ilikiwa Sh 95 lakini hivi sasa imepanda na kufikia Sh 3,150 akisema hatua hiyo imetengeneza matajiri wengi kwa kupanda kwa bei ya hisa.

Tuzo hizo za heshima zinalenga kuwatambua wafanyakazi na idara zilizofanya vizuri na kuwapa motisha kuonyesha benki yao inawathamini.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this