Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu

MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal ambaye pia amewaki kuwa kocha wa timu mbalimbali nchini, Athuman Bilali maarufu Bilo, amefariki dunia huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

Bilo ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika kukuza vipaji vya soka kwa vijana. Kipindi cha uhai wake alizinoa timu mbalimbali kama vile  Toto Africans, Pamba, Gwambina FC, Alliance FC, Stand United, ambapo hadi mauti yanamkuta alikuwa akimiliki timu ya soka ya wanawake inayoitwa Bilo Queens inayoshiriki Ligi Kuu Soka Wanawake Tanzania Bara. 

Meneja wa timu ya Bilo Queens, Elias Mwachula amethibitisha kufariki kwa mkurugenzi wao, akisema kuwa alipewa taarifa asubuhi.

Mwachula ameeleza kama wiki mbili zilizopita alikuwa na homa lakini hali yake iliimarika na kusema kuwa taarifa hizo kifo za bosi wake zilimpa mshtuko mkubwa kwa sababu jana walikuwa wote katika mazoezi ya timu na muda mwingi waliwasiliana kutokana na maandalizi ya safari ya timu yao waliyokuwa wakifanya.

“Tumepata pigo kubwa sana kuondokewa na mkurugenzi wetu, jana nilikuwa naye asubuhi mpaka jioni tunamaliza mazoezi. Tulikuwa na mpango wa kusafiri tarehe 19 kwenda Dar es Salaam kucheza na Ruangwa,” amesema meneja huyo.

spot_img

Latest articles

DAWASA YAREJESHA MAJI KIKONGO BAADA YA MIAKA MIWILI

Na Mwandishi Wetu WAKAZI takribani 1,500 wa Vijiji vya Lupunga, Videte na Kwa Mkino,...

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

SERIKALI KUANZA UTAFITI WA MADINI ENEO KUBWA LA NCHI KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI

Ni kupitia mfuko wa utafiti wa Madini ▪️Rais Samia apongezwa kwa dhamira ya kukuza sekta...

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMEME IGANJO, MBEYA

📌 Ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 93 ya utekelezaji 📌 Aeleza manufaa ya mradi...

More like this