Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani: TRA Yakabidhi Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Milioni 40

Na Tatu Mohamed

KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za afya katika hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema tukio hilo ni ishara ya matendo ya huruma na mshikamano kati ya taasisi za serikali na jamii.

“Tume­kutana hapa kwa ajili ya matendo ya huruma ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamekabidhi vifaa tiba kwa ajili ya Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam. Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na wanaDar es Salaam wote, tunatumia nafasi hii kuwashukuru TRA kwa kitendo hiki walichokifanya,” amesema Mpogolo.

Ameongeza kuwa pamoja na msaada huo, TRA imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya serikali, jambo ambalo linaendelea kuchangia maendeleo ya taifa.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja wa fedha 2025/2026, TRA imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 32 sawa na asilimia 103.7 ya lengo, jambo linaloonesha mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato,” amesema Mpogolo.

Amefafanua kuwa, pamoja na mafanikio hayo, TRA haijaishia kukusanya mapato pekee bali imeamua pia kurejesha sehemu ya rasilimali zake kwa jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii.

Amesema pia TRA imeendelea kuboresha mifumo ya ulipaji kodi ili kurahisisha huduma kwa walipa kodi pamoja na kuanzisha dawati maalumu linalowezesha walipa kodi kukutana na mamlaka hiyo kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Mcha Hassan Mcha amesema msaada huo wa vifaa tiba ni sehemu ya mchango wa taasisi hiyo kwa jamii wakati dunia ikielekea kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Amesema TRA imeamua kusogea karibu zaidi na jamii kwa kutoa mchango wa moja kwa moja katika kutatua changamoto za kijamii ikiwemo sekta ya afya.

“Hii inaongeza imani na mtazamo chanya wa wananchi kwa taasisi na serikali pamoja na walipa kodi, na inaonesha namna tunavyotambua mchango wa walipa kodi katika maendeleo ya taifa,” amesema.

Ametumia pia fursa hiyo kuwashukuru walipa kodi wote kwa mchango wao katika maendeleo ya nchi, akibainisha kuwa mbali na jukumu la kukusanya mapato, TRA pia ina wajibu wa kujenga uhusiano mzuri na jamii.

Naye Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA, Feliciana Nkane, akiwawakilisha wanawake wa TRA, amesema taasisi hiyo imeanza maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa vitendo kwa kugusa maisha ya wananchi.

Amesema jana walizindua Jukwaa la Wanawake na Kodi ambalo linalenga kutoa elimu ya kodi kwa lugha rahisi kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake nchini ili kuwasaidia kukuza biashara zao na hatimaye kuwa rasmi na kuchangia uchumi wa taifa.

“Sisi wanawake watumishi wa TRA tumeona ni vyema kusherehekea siku hii kwa vitendo kwa kugusa maisha ya wananchi wenzetu. Ndiyo maana leo tumekusanyika hapa kukabidhi vifaa tiba vitakavyosaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi,” amesema Feliciana.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk. Frank Chiduo amesema vifaa hivyo vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuzipunguzia changamoto baadhi ya vituo vya afya.

“Suala hili limekuja wakati muafaka hasa katika kipindi ambacho serikali imeanzisha mpango wa bima ya afya kwa wote, hivyo vifaa hivi vitakuwa msaada mkubwa katika kuboresha utoaji wa huduma,” amesema Dk. Chiduo.

Mwisho

spot_img

Latest articles

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa...

Vunjabei, Sara kuisaka heshima ya Tanzania One ulingoni

Na Winfrida Mtoi MABONDIA wa ngumi za kulipwa, Halima Ramadhani maarufu Vunjabei na Sara Alex...

More like this

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa...