Na Mwandishi Wetu
NYOTA wa zamani wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Yacouba Songne, ametambulishwa rasmi na klabu ya Mbeya City akiwa miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo msimu huu ili kuimarisha kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mecky Mexime.
Yacouba raia wa Burkina Faso, amereja tena Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukaa nje karibia nusu msimu kutokana kujitibia jeraha la goti. Amewahi kuzitumia klabu za Ihefu, Tabora United.
Wachezaji wengine walitua Mbeya City kipindi cha dirisha dogo ni Said Naushad, Hijja Shamte waliwahi kuitumikia Kagera Sugar na Abdallah Kulandana, akitokea Fountain Gate FC.


