Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu

Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2025/26.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Laizer amewashinda Zedekia Otieno wa Tanzania Prisons na Francis Baraza wa Pamba Jiji alioingia nao fainali katika mchakato huo.

Kocha huyo aliiongoza Fountain Gate katika michezo miwili na kujikusanyia alama saba, ikiwa na jumla ya mabao mawili ya kufunga na hajaruhusu bao na kuisaidia timu kutoka nafasi ya 14 hado sita katika msimamo wa ligi hiyo.

Pia kiungo wa timu hiyo Issa Abushiri, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba alitoa mchango katika michezo ya timu yake, akifunga bao moja  ambapo Fountain Gate Ilishinda bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji na ikashinda bao 1-0 dhidi ya KMC na  sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union.

Wakati huohuo Kamati ya Tuzo za TFF, imemchagua Rishedy Kihedu wa Mbuni FC kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba wa Ligi Championship ya msimu wa  2025/26, huku Leonard Budeba pia wa Mbuni FC akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Jackson Mwendwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Oktoba, kutokana na kufanya vizuri katika meneji-menti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this