Heche viongozi wengine Chadema waachiwa na Polisi kwa dhamana

Na Mwandishi Wetu

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche na viongozi wengine wa chama hicho  wameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi jioni ya leo jumatatu Novemba 10, 2025.

Heche ameachiwa pamoja na viongozi wengine wa chama hicho akiwemo Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa, Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani Boniface Jacob na Mjumhe wa Kamati Kuu Godbless Lema.

Kwa mujibu wa wakili Hekima Mwasipu amesema Heche ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi toka Oktoba 22, 2025 alipokamatwa katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Amesema viongozi wote hao wameachiwa katika kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam

spot_img

Latest articles

Rais Mwinyi azindua Baraza la Wawakilishi, ataja mwelekeo wa Serikali atakayounda

Na Mwandishi Wetu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na...

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

More like this