Na Winfrida Mtoi
Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ikipindua meza kwa kuifunga Silver Strikers mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
Mabao ya yaliyoipa ushindi Wanajangwani hao, yamefungwa na Dickson Job dk 06 na Pacome Zouzoua dk 34. Katika mchezo wa kwanza ulipigwa nchini Malawi, Yanga ilipoteza kwa kufungwa na Silver Strikers 1-0.


