Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi

Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya Simba imetamba kuwa ni kati ya timu tatu Afrika zenye uhakika wa kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 21,2025 na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally wakati akizungumza na waandishi kuelekea mchezo wao wa marudiano na  Nsingizini inayotokea Eswatini,  wakisaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi. Mechi hiyo itachezwa Jumapili hii Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa wana sababu zote za kuonyesha utofauti kwa kuwa ndiyo timu pekee kutoka Tanzania iliyopata ushindi ugenini katika michezo ya mkondo wa kwanza raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika. “Afrika hii timu zenye uhakika wa kucheza makundi mara saba mfululizo ni Al Ahly na Mamelodi na sisi tunaongezeka hapo.

“Tulikuwa tunapiga kelele kwamba Simba yetu hatuelewi inavyocheza lakini sasa imerejea. Simba ya kutisha imerejea, Simba ya kushambulia muda wote imerejea sasa unabaki nyumbani kufanya nini. Na haya sio maneno ya kutoka usingizi, haya ni maneno ya kuona inacheza na pale mwalimu anasema uwanja ulikuwa mdogo. Sasa uwanja wa Mkapa anakwenda kwenye uwanja mkubwa, njoo Uwanja wa Mkapa uone Simba ikifanya balaa zito, amejinasibu Ahmed.

Amesema mchezo huo pia itakuwa ni nafasi pekee kwa mashabiki kuona  uhalisia wa kocha wao mpya  Dimitar Pantev ambaye licha ya ushindi lakini alisema bado hajaridhishwa na kiwango cha timu yake.

spot_img

Latest articles

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

More like this

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...