Na Mwandishi Wetu
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mchezo wake dhidi ya Niger uliopigwa leo Septemba 9, 2025 katika Dimba la New Amani Complex Zanzibar kwa kufungwa bao 1-0
Kwa kichapo hicho Taifa Stars wanasalia nafasi ya pili kundi E ikiwa na pointi 10, Morocco ndiyo inaongoza na tayari imeshafuzu kucheza Kombe la Dunia, huku Niger ikiwa nafasi ya tatu na alama tisa.
Stars ilihitaji ushidi leo ili kuwa na matuini ya kucheza hatua ya mchujo, Wiki iliyopita ilitoka sare ya 1-1 ugenini na Congo Brazaville ugenini hali inayoiweka katika ugumu.



