Serikali yaondoa pingamizi shauri la Mpina, kesi kusikilizwa Jumatatu

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma imepanga kusikiliza kesi ya ACT Wazalendo na Luhanga Mpina dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jumatatu Septemba 8,2025.

Shauri hilo limesikilizwa  leo Septemba 3,2025 kwa njia ya mtandao mbele ya jopo la Majaji watatu, Jaji  Evaristo Longopa, Jaji John Kahyoza na Jaji Abdi Kagomba  ambapo Mahakama imeridhia kesi hiyo isikilizwe  ndani ya siku tano kwa njia ya maandishi , huku Mawakili wa pande zote mbili wakitarajiwa takutana Mahakamani kufanya mjumuisho wa hoja zilizowasilishwa kwa maandishi mahakamani hapo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa ACT Wazalendo, upande wa Serikali umeamua kuondoa mapingamizi waliyokuwa wameweka awali kuhusiana na kesi hiyo, hatua ambayo imeongeza urahisishaji wa kusikiliza kesi ya msingi.

Kesi hiyo namba 21692/2025, iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa ACT Wazalendo pamoja na Lugaha Mpina, ikipinga uamuzi wa INEC kumuengua mgombea wao  wa Urais, katika orodha ya wagombea.

spot_img

Latest articles

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...

More like this