DKT. KIKWETE APONGEZA HUDUMA YA MAJI CHALINZE, AIPA USHAURI DAWASA

Na Mwandishi Wetu

RAIS Mstaafu, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuangalia uwezekano wa kujenga Bwawa Dogo eneo la Wami, litakalosaidia kuongeza upatikanaji wa maji Chalinze ifikapo mwaka 2030 hadi 2050.

Akizungumza baada ya kutembelewa na Meneja wa DAWASA Chalinze, Mhandisi Boniface Ole Philemon, nyumbani kwake, Msoga- Chalinze, Dkt. Kikwete amesisitiza mahitaji ya maji yanaongezeka kutokana na ongezeko la watu na viwanda, hivyo maandalizi ya muda mrefu yanahitajika.

Pia, ameshauri mazungumzo yafanyike na mashamba ya Mtibwa, mkoani Morogoro, kubaini kiasi cha maji wanachotumia ili kuwezesha maji mengi zaidi kufika mto Wami.

Aidha, amependekeza matumizi ya maji kwa Bagamoyo Sugar yazingatiwe.Dkt. Kikwete amefurahishwa na hali ya huduma ya maji Mji wa Chalinze na kupongeza kazi inayofanywa na Wizara na DAWASA, na kusema kazi kubwa imefanyika chini ya Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso na watumishi wote wa Sekta ya Maji Nchini.

Dkt. Kikwete amesema kwa sasa hapokei malalamiko kuhusu huduma ya maji Chalinze na amesisitiza kazi nzuri inayoendelea iendelezwe, huku mapendekezo yake yakilenga kuimarisha upatikanaji wa maji kwa mahitaji yajayo.

spot_img

Latest articles

DAWASA YAREJESHA MAJI KIKONGO BAADA YA MIAKA MIWILI

Na Mwandishi Wetu WAKAZI takribani 1,500 wa Vijiji vya Lupunga, Videte na Kwa Mkino,...

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

SERIKALI KUANZA UTAFITI WA MADINI ENEO KUBWA LA NCHI KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI

Ni kupitia mfuko wa utafiti wa Madini ▪️Rais Samia apongezwa kwa dhamira ya kukuza sekta...

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMEME IGANJO, MBEYA

📌 Ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 93 ya utekelezaji 📌 Aeleza manufaa ya mradi...

More like this