MKAKATI WA PAMOJA KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUONGEZA IDADI YA WATUMIAJI- WAZIRI HOMERA

📌Aongoza Site Trust Nishati safi Marathon Namtumbo, Ruvuma

📌Aipongeza TANESCO kwa mpango wa ukopeshaji majiko, ahimiza elimu hiyo ifike mbali zaidi

📌Akabidhi gari kwa TANESCO Namtumbo kusogeza huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nishati, Dkt Juma Homera amesema mkakati wa pamoja wa kuelimisha matumizi ya nishati safi ya kupikia utachangia idadi kubwa ya wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo sio salama hivyo kufanikisha kwa vitendo malengo ya Serikali ya kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi.

Homera ameyasema hayo leo, Oktoba 24, 2026, wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma, wakati akiongoza mbio za Site Trust Nishati Safi Marathon 2026, zilizolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza katika Banda la TANESCO Waziri Homera amesema kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034 ni jukumu linalohitaji mikakati madhubuti na ushirikiano wa wadau mbalimbali ili kuhamasisha wananchi kuachana na nishati zisizo salama na kuhamia kwenye nishati safi.

Ameipongeza TANESCO kwa kuanzisha mpango wa kuwawezesha wananchi kupata majiko yanayotumia umeme kwa kulipa kidogo kidogo kupitia manunuzi ya umeme wa LUKU.

Amesisitiza kuwa mpango huo unapaswa kutangazwa zaidi na kuwafikia wananchi wengi , hususan wanaoishi maeneo ya vijijini.

“TANESCO mnafanya kazi nzuri sana, si tu katika kutekeleza miradi ya umeme, bali pia kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme. Natoa rai kwenu, mpango huu wa ukopeshaji majiko kwa wananchi utangazwe kwa upana zaidi kwa kuwa unagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wa mijini na vijijini,” alisisitiza Homera.

Kwa upande wake, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Wadau wa TANESCO, Augustino Kasale, amesema Shirika linaendelea kutumia majukwaa mbalimbali kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme, ikiwemo matumizi ya majiko yanayotumia umeme kwa ufanisi, kwa lengo la kupunguza gharama za kupikia, kulinda afya za wananchi na kutunza mazingira.

“TANESCO inaendelea kutekeleza mpango wa ukopeshaji majiko kwa wananchi kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha, tunaendelea kutumia majukwaa mbalimbali kutoa elimu hiyo kama sehemu ya jitihada za kuunga mkono ajenda ya Serikali ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi. Mwitikio wa wananchi wanaohitaji na kutumia majiko haya ni mkubwa,” alifafanua Kasale.

Katika hatua nyingine, Waziri Homera alikabidhi gari kwa TANESCO wilayani Namtumbo kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za umeme kwa wananchi wa Tarafa ya Lusewa, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

Aidha, washindi wa mbio za Site Trust Nishati Safi Marathon 2026 walikabidhiwa majiko yanayotumia umeme kwa ufanisi ili kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuhusu faida za kutumia umeme kupikia.

spot_img

Latest articles

TANESCO KUIWEZESHA KAMPUNI YA HWTZ MEGAWATI 200 KUTEKELEZA MRADI WA UZALISHAJI UMEME

📌Waziri Homera afanya Ziara katika Kongani ya Viwanda Mkoani Ruvuma chini ya muwekezaji HWTZ...

TEKNOLOJIA YA NYUKLIA NI NYENZO YA MAENDELEO AFRIKA

Na Tatu Mohamed IMEELEZWA kuwa Sayansi na teknolojia ya nyuklia vinapaswa kutazamwa kama nyenzo za...

DKT. KIKWETE APONGEZA HUDUMA YA MAJI CHALINZE, AIPA USHAURI DAWASA

Na Mwandishi Wetu RAIS Mstaafu, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Mamlaka ya Majisafi...

DAWASA YAREJESHA MAJI KIKONGO BAADA YA MIAKA MIWILI

Na Mwandishi Wetu WAKAZI takribani 1,500 wa Vijiji vya Lupunga, Videte na Kwa Mkino,...

More like this

TANESCO KUIWEZESHA KAMPUNI YA HWTZ MEGAWATI 200 KUTEKELEZA MRADI WA UZALISHAJI UMEME

📌Waziri Homera afanya Ziara katika Kongani ya Viwanda Mkoani Ruvuma chini ya muwekezaji HWTZ...

TEKNOLOJIA YA NYUKLIA NI NYENZO YA MAENDELEO AFRIKA

Na Tatu Mohamed IMEELEZWA kuwa Sayansi na teknolojia ya nyuklia vinapaswa kutazamwa kama nyenzo za...

DKT. KIKWETE APONGEZA HUDUMA YA MAJI CHALINZE, AIPA USHAURI DAWASA

Na Mwandishi Wetu RAIS Mstaafu, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Mamlaka ya Majisafi...