Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ya 2025/26, ikitarajia kuanza rasmi Septemba 17, 2025 na kutamatika Mei 23, 2026,  huku mchezo wa Dabi ya Karikoo Yanga dhidi ya Simba utapigwa Desemba  13, 2025, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo wa raundi ya pili wa watani hao wa jadi ambao mwenyeji atakuwa Simba, utapigwa Aprili 04,2026 kwenye dimba uwanja huo.

Mechi za ufunguzi za msimu huu mpya, KMC itaikaribisha Dodoma Jiji Uwanja wa KMC Complex, Mwenge wakati Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons katika dimba la Mkwakwani, Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Ibrahim Mwayela amesema ratiba hiyo imezingatia kalenda ya mashindano yote ya ndani na Kimataifa ili kuhakikisha ligi hiyo inakwenda vizuri na kumalizika Mei 23, 2026 kama ilivyopangwa.

 “Ligi yetu inakwenda kuanza rasmi. Tunaamini utakuwa ni msimu mzuri wenye ushindani mkubwa kwa sababu timu zote zimejiandaa na zimesajili vizuri sana na maandalizi yanaendelea,” amesema.

Ratiba yote ya Ligi Kuu Tanzania Bara hii hapa https://www.ligikuu.co.tz

spot_img

Latest articles

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...

More like this