Geofrey Timothy achukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kawe

Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Geofrey Timothy, amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo na kuahidi kuwatumikia wananchi wa Kawe kwa ari na moyo wa kujituma.

Akizungumza leo Agosti 26, 2025 mara baada ya kuchukua fomu, Timothy ameishukuru CCM kwa imani waliyoonesha kwake kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa mwaka huu.

“Nashukuru viongozi wa Chama kwa kuniteua kupeperusha bendera ya chama kupitia Jimbo la Kawe. Yapo mengi tumepanga kuyafanya…nawashukuru wajumbe kwa kunipigia kura nyingi kupeperusha bendera ya chama,” amesema.

Aidha, Timothy amewataka wakazi wa Kawe kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni za CCM utakaofanyika Agosti 28, 2025, akisema utakuwa ni fursa ya wananchi kusikia kwa kina mipango ya chama na kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema Chama hicho kimejipanga kwa mikakati thabiti ya kuendeleza utekelezaji wa Ilani kwa vitendo, ikiwemo kuboresha huduma za kijamii, kuongeza ajira kwa vijana pamoja na kukuza fursa za kiuchumi.

spot_img

Latest articles

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

More like this