Kijana ahukumiwa jela miaka 30 kwa kubaka mzee wa miaka 80 kichakani

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, imemhukumu Said Nawanje (20) mkazi wa Yombo Lukinga, wilayani humo, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mzee wa miaka 80.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni Mosi, 2025 huko Kijiji cha Yombo Lukinga, Kisarawe baada ya kumvizia bibi huyo akitoka shambani ambapo alimtishia kisu kisha kumsukuma kichakani na kumbaka.

Hukumu hiyo ya kesi namba 15006/2005 imesomwa Agosti 20, 2025 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe, Simon Mosses baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Hakimu Mosses alieleza kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1), (2) (a) na 131 (1) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya...

More like this