Wizara yateua viongozi wa muda Kamisheni ya Ngumi

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, amemteua mwandishi wa habari, Patrick Nyembera kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC), baada ya kamati ya awali kumaliza muda wake.

Nyembera ataiongoza kamati hiyo ya muda ya TPBRC, yenye jumla ya wajumbe sita akiwamo Makamu wake Jacob Mbuya .

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara iliyotolewa leo Agosti 15, 2025 Profesa Kabudi ameipa kamati hiyo siku 90 (kuanzia Julai 29 hadi Oktoba 29) kukamilisha marekebisho ya katiba na kuitisha uchaguzi mkuu.

Wengine walioteuliwa  ni Gordon Nsajigwa (Katibu), wajumbe ni Shafii Dauda, Irene Mwasanga na Ibrahim Abbas Kamwe.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya...

More like this