Yanga yapelekwa Angola, Simba Botswana

Na Winfrida Mtoi

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga itaanza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola wakati Simba itacheza na Gaborone United ya Botswana.

Wababe hao wa Tanzania Bara wote wataanzia ugenini kati ya Septemba 19 na 21, 2025 na kurudiana kati ya Septemba 26 na 28, 2025 jijini Dar es Salaam.

Yanga ikipita hatua hiyo itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Algeci Plus ya Madagascar dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, huki Simba ikivuka hatua itacheza na mshindi wa mchezo wa Bhora ya Zimbabwe na Nsingizia Hotspurs ya Eswatin.

Wawakilishi wa Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Mlandege itaanzia ugenini ikicheza na Insurence ya Ethiopia.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho Azam FC itaanzia nyumbani dhidi ya El Merrekh Bantiu ya Sudan Kusini, Singida Bs wamepangwa kucheza na Rayon Sports ya Rwanda, wakati KMKM ya Zanzibar itacheza na AS Port ya Djibouti ambapo zote zitaanzia ugenini.

Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho imefanyika leo Agosti 9, 2025 jijini Dar es Salaam na kushudiwa na viongozi mbalimbali wa soka hapa nchini na Afrika.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this