Mbaroni kwa kumuua mama mkwe na kumjeruhi mkewe

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Jumanne Kibagi, mkazi wa kijiji cha Nyarufu wilayani Bunda kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wake  iatwaye  Kabula Masanja (50) na kumjeruhi mkewe  Nyangeta Kunyaranyara (21) kwa kutumia panga.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, tukio hilo limetokea Julai 19, 2025  majira ya saa  7;30 usiku katika kijiji cha Chumwi kilichopo wilayani Musoma, ambapo chanzo kimetajwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia kati ya mtuhumiwa na mke wake.

Inadaiwa kuwa  Nyangeta ambaye ni mke wa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mume wake kujihusisha na  vitendo vya kihalifu hususani wizi hali iliyosababisha mwanamke huyo kukimbilia nyumbani kwa mama yake ambapo mtuhumiwa aliwafuata huko  na kuwashambulia kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali.

“Majirani walifanya jitihada za kuwapeleka katika kituo cha afya Murangi kwa  jailli ya kupatiwa matibabu ambapo Kabula Masanja alifariki akiwa anaendelea na matibabu,” imesema taarifa hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, mke wa mtuhumiwa, Nyangeta, akiwa katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alikolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ameeleza kuwa mtuhumiwa alifika nyumbani kwao usiku na kutekeleza tukio hilo.

Amesema Jumanne alikuwa mume wake ambaye waliishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja, na waliachana baada ya kugundua mwanaume huyo anajihusisha na matukio ya kihalifu.

Nyangeta amesema kabla ya tukio hilo, Jumanne alimpigia simu mama yake akimjulisha nia ya kwenda kumchukua mke wake (Nyangeta), ambapo mama yake alikataa, na ndipo siku ya tukio alipovamia na kuwakata panga yeye na mama yake.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this