JAB yawafungia watangazaji wanne wa kipindi cha Genge la GEN TOK kwa kukiuka maadili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewafungia watangazaji wanne wa kipindi cha redio kinachojulikana kama ‘GENGE LA GEN TOK’ kwa kosa la kukiuka sheria na maadili ya taaluma ya habari.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 18, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Patrick Kipangula imewataja watangazaji hao ni Deodatha William, Mussa Crispin Mgenge, Perfect Crispin na Iddy Bakari Iddy ambao walikiuka taratibu katika kipindi kilichorushwa Julai 16, 2025 kwa kufanya mahojiano yaliyojaa lugha ya kudhalilisha, kushusha utu wa mhojiwa na kumlazimisha kutoa taarifa binafsi bila ridhaa yake.

Mhojiwa katika kipindi hicho alikuwa msanii wa muziki wa Singeli anayefahamika kwa jina la Dogo PATEN.

Taarifa hiyo ya JAB imesema kuwa watangazaji hao walifanya kazi bila Ithibati, kinyume cha Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari (Toleo la 2023), jambo ambalo ni kosa kisheria.

Bodi imesema uchambuzi wake wa kitaalamu umebaini kuwa watangazaji hao walikiuka Kanuni za Mawasiliano kwa kutumia lugha isiyo na staha na kuhoji kwa mtindo unaodhalilisha utu wa mtu, kinyume na maadili ya utangazaji wa redio na televisheni kama yalivyofanyiwa marekebisho mwaka 2018 na 2020.

“Kutokana na ukiukwaji huo, JAB imeamua kuwapiga marufuku watangazaji hao kujihusisha na kazi yoyote ya habari kuanzia tarehe ya taarifa hii hadi watakapokidhi vigezo vya kupata Ithibati na kuthibitisha kuwa wana sifa za kitaaluma na kimaadili,” ameeleza taarifa hiyo.

Bodi hiyo pia imetoa onyo kwa vyombo vyote vya habari nchini kuhakikisha wanawaajiri watu wenye sifa na waliothibitishwa kisheria, huku ikisisitiza umuhimu wa kufuata maadili, weledi na heshima katika kazi ya uandishi wa habari.

“Uhuru wa habari unakwenda sambamba na wajibu wa kufuata sheria na kuheshimu utu wa binadamu,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...