Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuhusu upatikanaji wa huduma ya majisafi mara baada ya kutembelea na kukagua maboresho yaliyofanyika katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu.

Akizungumza mara baada ya kukagua Mtambo huo, Waziri Aweso amesema: “Kwakweli hali inaridhisha sasa, nilitoa maagizo ya maboresho katika mtambo huu, leo nimekuja kujionea, nitoe pongeze kwa Menejimenti ya DAWASA kazi kubwa imefanyika hapa na katika chanzo tumekuta maji ya kutosha kabisa,”.

Aweso ameongeza kwa kutoa maelekezo kwa DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji bila kikwazo chochote kwani hali ya mtambo ni nzuri na maji yapo yakutosha.

“Maji haya sasa ni wajibu wa DAWASA kuhakikisha yanawafikia wananchi na kunufaika nayo, Wizara itaendelea kuwapa ushirikiano kuhakikisha hamkwami, lakini pia ili kuboresha huduma Serikali imeasha agiza pampu mpya katika mtambo huu ili ziwe mbadala pale kunapotokea hitilafu” amesema Aweso.

Ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Pwani pamoja na Chama Cha Cha mapinduzi (CCM) kwa ushirikiano wa kutosha kwa Wizara hali inayofanya huduma ya maji kuwa ya uhakika.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya maji, Mhandisi Mwajuma Waziri ameipongeza DAWASA Kwa maboresho makubwa waliyofanya na kuwataka kuhakikisha wanawasikilza wananchi ili kuondoa malalamiko huku wakihakiksha wanapambana na upotevu wa maji kwa kudhibiti mivujo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon ameeleza kuwa wanashirikiana kwa karibu na DAWASA na Bonde Wami-Ruvu katika utafutaji wa vyanzo mbadala vitakavyosaidia kuzuia uharibifu katika chanzo Cha mto Ruvu ikiwemo ujenzi wa birika za kunyweshea mifugo katika vijiji vya Minazi Mikinda na Mpera-mumbi.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire ameeleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2025 – 2026 Mamlaka imewekeza nguvu kubwa katika kuwaungia wananchi huduma ya maji ambapo imelenga kuunganisha wateja wapya 72,000.

spot_img

Latest articles

Dk. Mwigulu ajadiliana na Kamati ya Maandalizi AFCON 2027

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi...

Coastal Union yawatembezea kichapo maafande wa Magereza

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Coastal Union imetembeza kichapo cha mabao 4-1 kwa maafande wa...

Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna...

Msajili wa Hazina aikaribisha Jeune Afrique Media Group kuangazia fursa za uwekezaji

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Frederic...

More like this

Dk. Mwigulu ajadiliana na Kamati ya Maandalizi AFCON 2027

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi...

Coastal Union yawatembezea kichapo maafande wa Magereza

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Coastal Union imetembeza kichapo cha mabao 4-1 kwa maafande wa...

Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna...