VETA yajivunia mageuzi makubwa, yazidi kuwanufaisha Watanzania

Na Tatu Mohamed

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema inajivunia mafanikio makubwa iliyoyapata katika mageuzi ya sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi, ambayo yamewezesha Watanzania wengi kupata ujuzi, kujiajiri na kuajiriwa katika sekta mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasole alisema taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo yanayolenga kumgusa Mtanzania wa kawaida.

“Kwa sasa VETA inatoa mafunzo katika maeneo mbalimbali, ikiwemo huduma kwa wazee majumbani ambapo zaidi ya watu 700 wamehitimu mafunzo hayo na kupata ajira,” alisema CPA Kasole.

Ameeleza kuwa mafanikio hayo yanatokana na msisitizo mkubwa uliowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha elimu ya mafunzo na ufundi stadi nchini.

“Msisitizo wa Rais umetuwezesha kutekeleza mambo mengi makubwa, yakiwemo ujenzi wa vyuo vipya. Kwa sasa tunavyo vyuo 80 na Serikali iko katika hatua ya kukamilisha vyuo vingine 65, ambavyo vimefadhiliwa na fedha zilizotolewa na Rais Samia,” alisema.

Kasole alibainisha kuwa kukamilika kwa vyuo hivyo kutaiwezesha VETA kuwa na jumla ya vyuo 145 nchini, hatua ambayo itahakikisha kila wilaya inakuwa na chuo cha VETA kwa ajili ya kutoa elimu ya ujuzi kwa wananchi kwa urahisi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alisema VETA imeanzisha kampuni tanzu inayolenga kukuza na kuendeleza bidhaa bunifu zinazotengenezwa kupitia vyuo vyao.

“Kampuni hiyo tanzu itasimamia bidhaa zote zinazozalishwa na wanafunzi wetu kutoka vyuo mbalimbali, ikiwemo fanicha, huduma za usimamizi wa miradi na kazi nyingine bunifu zitakazouzwa kupitia kampuni hiyo,” alisema CPA Kasole.

Alisema hatua hiyo inalenga kuwapa wanafunzi uzoefu wa moja kwa moja katika mazingira ya kibiashara sambamba na kuchochea ubunifu unaozingatia mahitaji ya soko.

Mwisho 

spot_img

Latest articles

NIT yaendelea na mafunzo ya Urubani, yawataka vijana kuchangamkia fursa

Na Tatu Mohamed CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeanza rasmi kutoa mafunzo ya...

TPDC yapata Tuzo ya Taasisi Bora Sabasaba kwa miaka mitano mfululizo

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeandika historia kwa kutwaa tuzo...

Rais Mwinyi atembelea Banda la ETDCO Sabasaba

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...

GF Trucks yaibuka mshindi wa jumla maonesho ya Sabasaba 2025

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Gf Trucks & Equipment imeibuka mshindi wa jumla katika Maonesho...

More like this

NIT yaendelea na mafunzo ya Urubani, yawataka vijana kuchangamkia fursa

Na Tatu Mohamed CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeanza rasmi kutoa mafunzo ya...

TPDC yapata Tuzo ya Taasisi Bora Sabasaba kwa miaka mitano mfululizo

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeandika historia kwa kutwaa tuzo...

Rais Mwinyi atembelea Banda la ETDCO Sabasaba

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...