Dk.Jingu awashauri vijana kujiandaa kwa uzee

Na Mwandishi Wetu

‎Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. John Jingu, ametoa wito mahsusi kwa vijana na jamii kwa ujumla kujiandaa kwa maisha ya uzee kwa kutumia vizuri rasilimali walizonazo. 

“Ni muhimu vijana wawe na mtazamo wa muda mrefu kwa kuwekeza katika familia, mahusiano mema na miradi ya kiuchumi ambayo itawasaidia wanapoingia uzeeni. Ujana ni hatua ya maandalizi ya uzee, tusikimbie wajibu huu,”

Dk. Jingu ameyasema hayo Julai 03, 2025 alipotembelea Makazi ya Wazee cha Bukumbi yaliyopo mkoani Mwanza kwa lengo la kuwajulia hali wazee wanaoishi katika Makazi hayo pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Aidha ameitaka jamii kushiriki kikamilifu katika kuwatunza wazee wao, kuwaheshimu, kuwaangalia na kulinda dhidi ya vitendo vya kikatili.

‎Katika ziara hiyo, Dk. Jingu amehimiza pia wazee kushiriki katika Uchaguzi Mkuu pamoja na fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo zile zinazotolewa kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). 

‎Katika hatua nyingine,ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mahabusu ya watoto jijini Mwanza ambapo ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa kwani mradi huo umefikia asilimia 90 ya utekelezaji. Ujenzi wa mahabusu hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya Tume Maalum iliyoundwa ili kuboresha Taasisi za haki jinai nchini hususan zinazohusiana na watoto.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this