Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu ya kugombea Udiwani Viti Maalumu Manispaa ya Ilala.
Mchau amekabidhiwa fomu hiyo leo Julai 1,2025 na Katibu Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Ofisini kwake Ilala Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Mchau amewaomba wanawake wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu ili kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani CCM ina demokrasia ya kutosha.