Rais Samia ataja mafanikio Sekta ya Nishati 2020-2025

📌Ni wakati akihitimisha shughuli za Bunge jijini Dodoma

📌JNHPP, Umeme Vijijini, Umeme wa Gridi Kigoma na Katavi; Ni baadhi ya Vielelezo vya mafanikio

📌 Ataja miradi mikubwa ya usafirishaji umeme iliyokamilika

📌Ataka TANESCO kuanza kuiangalia Nyukilia kama moja ya vyanzo vya kuzalisha umeme nchini

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Sekta ya Nishati imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitano.

Ameyasema hayo wakati akihitimisha shughuli za Bunge Jijini Dodoma tarehe 27 Juni 2025.

“Mheshimiwa Spika kutokana na umuhimu wa Sekta ya Nishati kwa maendeleo ya nchi, Serikali imeimarisha upatikanaji wa nishati nchini ikiwemo kukamilisha mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP),” amesema Samia.

Ameongeza kuwa, mbali ya kukamirisha mradi wa Julius Nyerere pia Serikali imekamilisha upelekaji wa umeme katika Vijiji vyote 12,318 nchini.

Amesema msukumo uliofanywa na Serikali katika sekta ya nishati umewezesha uzalishaji wa umeme kuongezeka hadi kufikia megawati 4031.71 kutoka megawati 1,601.84 mwaka 2020.

“Hali hii imechangiwa na miradi mbalimbali ya uzalishaji umeme ukiwemo mradi wa kielelezo wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere wenye megawati 2115, vilevile mradi wa Kinyerezi I Extension wa megawati 185 na mradi wa Rusumo ambao tumeutekeleza kwa ushirikiano wa Nchi tatu za Tanzania, Burundi na Rwanda kwa mgawanyo wa megawati 26.67 kwa kila Nchi,” amesema Rais Samia.

Katika miradi ya usafirishaji umeme amesema Serikali imekamilisha miradi ya usafirishaji umeme ya kutoka Singida hadi Arusha, Geita hadi Nyakanazi, na Julius Nyerere hadi Chalinze.Miradi mingine ni Nyakanazi hadi Kigoma, Tabora hadi Urambo, Rusumo hadi Nyakanazi na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kwenye njia ya Reli.

Amesema mafanikio hayo yameongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo mbalimbali nchini.Aidha ameeleza kuwa, Serikali imefanikiwa kuiunganisha mikoa ya Kigoma na Katavi na gridi ya Taifa.

Kuhusu umeme Vijijini, Rais Samia amesema Tanzania imefikia hatua kubwa na ya kihistoria kwa kuunganisha Vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara na huduma ya umeme.

Amesisitiza kuwa, kwa sasa Serikali inapeleka umeme kwenye Vitongoji ambapo vitongoji 33,657 tayari vimeshafikishiwa umeme kati ya Vitongoji 64,359 sawa na asilimia 52.3.

Kuhusu nishati mbadala, amesema Serikali inampango wa kuzalisha nishati mbadala kwa kutumia vyanzo jadidifu ambapo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kuanza kufikiria kuanza kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Nyukilia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema Serikali inapanga kuweka ushindani katika Sekta ya nishati kwa kuialika sekta binafsi kushiriki kuongeza upatikanaji wa umeme.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...