Mwanamke ajiua kwa sumu  kisa mapenzi

Na Mwandishi Wetu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Richard Abwao,  amesema mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Catherine Fito, mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Umanda Kata ya Kalunde Manispaa ya Tabora, amejiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu, huku chanzo cha kifo hicho ikiwa ni wivu wa mapenzi.

Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda  Abwao, amesema limetokea Juni 14,2025, ambapo mwanamke huyo anadaiwa kuwa katika mgogoro na mwenza wake kwa muda, hali iliyofanya kuchukua uamuzi huo.

“Tuna tukio moja la mwanamke kujiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu huko katika kijiji cha Umanda, Kata ya Kalunde Manispaa ya Tabora, aliyetambulika kwa jina la Catherine Fito mwenye umri wa miaka 21, ilipofika saa nne usiku siku ya tarehe 14 Mume wa marehemu alifika nyumbani kwake na kumkuta mwanamke huyo anagalagala chini nje  akiwa anatapika na alipumuuliza akajibu amekunywa sumu ya kuulia wadudu.

“Mgonjwa alipatiwa huduma ya kwanza katika zahanati ya Umanda na baada ya hapo akapewa Rufaa ya kwenda hospitali ya Milambo, lakini hawakufanya hivyo ndugu zake wakamchukua kumrudisha nyumbani na ilipofika saa kumi na mbili jioni siku ya tarehe 15 akafariki dunia akiwa nyumbani kwake na chanzo cha kifo hiki ni wivu wa kimapenzi.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this