Tanesco yashinda Tuzo ya uhifadhi wa Mazingira kupitia Mradi wa JNHPP

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya uhifadhi wa mazingira katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma leo tarehe 05 Juni, 2025.

Tuzo hiyo imetolewa kutambua mchango wa TANESCO katika kuhifadhi mazingira kupitia utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ambao umeendelea kuzingatia misingi ya utunzaji wa mazingira sambamba na kuchangia kupunguza gesi joto.

Tuzo hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, katika hafla ya kufunga rasmi maadhimisho hayo.

Kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, TANESCO imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kutekeleza miradi mikubwa ya umeme kwa kuzingatia usalama wa mazingira, ikiwa ni pamoja na JNHPP na mingine inayolenga kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

spot_img

Latest articles

Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na...

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

More like this