Mradi wa EACOP wafikia asilimia 60 ya utekelezaji

Na Mwandishi Wetu

UTEKELEZAJI wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP), unaojumuisha ujenzi wa bomba la urefu wa kilomita 1,443 kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga – Tanzania, umefikia asilimia 60 ya utekelezaji.

Taarifa hiyo ilitolewa Juni 2, 2025, wakati Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipofanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo katika eneo la Chongoleani, mkoani Tanga.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati, Mhandisi Ngosi Mwihava, alieleza kuridhishwa kwa bodi na maendeleo ya mradi huo.

Alisisitiza kuwa EWURA ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa mradi huu sambamba na kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa za ajira, uhamishaji wa ujuzi na teknolojia, pamoja na upatikanaji wa fursa za kibiashara zinazohusiana na utoaji wa bidhaa na huduma.

Akitoa ufafanuzi zaidi, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Huduma za Utawala wa Kampuni ya EACOP, Geoffrey Mponda, alisema kuwa hadi sasa mradi huo umetoa ajira kwa watu zaidi ya 6,000, ambapo takriban asilimia 70 ni wakazi wa maeneo yanayozunguka mradi huo, jambo linaloonyesha kuimarika kwa ushiriki wa wazawa katika mradi huo.

Mapema kabla ya kutembelea mradi, Bodi ya EWURA ilikutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi, Dkt. Batilda Salha Burian, ambaye alieleza kuwa mradi wa EACOP umeleta manufaa makubwa kwa wakazi wa mkoa huo, na kwamba wazabuni wengi wa ndani wamejisajili kwenye kanzidata ya watoa huduma inayosimamiwa na EWURA.

Serikali ya Tanzania inamiliki asilimia 15 ya hisa za mradi kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this