TMA yapata ugeni kutoka Zimbabwe kujifunza masuala mbalimbali ya Hali ya Hewa Tanzania

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepokea ugeni kutoka Idara ya Huduma za Hali ya Hewa ya Zimbabwe (MSD), waliokuja nchini kwa ziara ya mafunzo ili kujifunza kuhusu masuala mbalimbali ya huduma za hali ya hewa.

Ugeni huo umeichagua TMA kwa kutambua mchango na mafanikio makubwa ya mamlaka hiyo katika kuimarisha huduma za hali ya hewa, si tu kwa Tanzania bali pia kwa bara la Afrika kwa ujumla.

KUHUSU TMA

TMA ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na. 2 ya mwaka 2019, kupitia Tangazo la Serikali Na. GN 459 la tarehe 14 Juni 2019.

Mamlaka hii ina jukumu la kuratibu, kudhibiti na kutoa huduma za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali, huduma za hali ya hewa nchini zilitolewa na Wakala wa Hali ya Hewa Tanzania, uliokuwa umeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala (Executive Agencies Act), Sura Na. 245, marejeo ya mwaka 2022.

Kabla ya kuanzishwa kwa wakala, huduma hizo zilitolewa na Idara ya Hali ya Hewa (Directorate of Meteorology) iliyoundwa mwaka 1977, kufuatia kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Idara hiyo ilitekeleza jukumu la kutoa taarifa na uangalizi wa hali ya hewa nchini.Kabla ya hapo, huduma hizo zilitolewa chini ya taasisi ya wakoloni waliokuwa wakitawala wakati huo.

TMA ipo chini ya Wizara ya Uchukuzi na inasimamia Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kilichopo Kigoma, ambacho hutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wataalamu whali ya hewa nchini.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

More like this