Spika wa Bunge ateta na Dk. Mwapinga, amhakikishia ushirikiano

Na Mwandishi Wetu

Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, amemhakikishia ushirikiano Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR), Dk. Deo Mwapinga katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

Dk, Tulia ameyasema hayo leo Mei 8, 2025 wakati alipomkaribisha  kufanya mazungumzo na  Dk. Deo Mwapinga, ofisini kwake Bungeni, Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Tulia amempongeza Dk. Mwapinga kwa kuchaguliwa katika wadhifa huo muhimu wa  kuliongoza Jukwaa hilo na kusisitiza   dhamira ya Tanzania kuendelea kushirikiana na taasisi za kikanda  kukuza demokrasia, utawala bora na maendeleo endelevu.

Dk. Mwapinga alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa FP-ICGLR Aprili 25, 2025 katika kikao cha juu cha Maspika wa Mabunge ambayo ni Wanachana wa Jukwaa hilo kilichofanyika Luanda, Angola.

Kwa  mujibu wa Katiba ya Jukwaa hilo ataongoza taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu , ikiwa ni nafasi inayoweza kurejewa.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this