Msigwa: Serikali itafanyia kazi haraka maazimio ya kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema itahakikisha inafanyia kazi mapendekezo yote yatakayotolewa kwenye maazimio ya pamoja ya Waandishi wa Habari baada ya kuhitimisha Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa mwaka 2025.

Hakikisho hilo la Serikali limetolewa Aprili 28, 2025 na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson wakati akitoa neno la kufunga Siku ya Kwanza ya Kongamano hilo linalofanyika jijini Arusha kwa uratibu wa Jamii Africa, UNESCO na Wizara yenyewe.

“Nimesikia maazimio ya awali mliyoyatoa hapa, ni muhimu sana na mimi nitaomba mkishakamilisha ile nakala ya mwisho mtupatie ili na sisi serikalini yale ambayo tunatakiwa tuchukue hatua tuyafanyie kazi, basi tutafanyia kazi mara moja”, amesema Msigwa.

Amewapongeza wadau wote walioshiriki Kongamano hilo na kwa majadiliano waliyoyafanya ikiwemo suala la matumizi ya Akili Mnemba kwa kuwa ni jambo muhimu kwenye kazi za uandishi wa habari kwa sasa.

Msigwa amesema Serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari nchini na kwamba hilo linajidhihirisha kwani kumekuwa na mazingira rafiki kwa Waandishi wa Habari pale wanapotekeleza majukumu yao.

“Sisi Waandishi wa Habari kwenye Awamu hii ya sita tumekuwa tukifanya kazi katika mazingira rafiki sana, kwa sababu ya maelekezo ambayo Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) anayasimamia,” amesisitiza Msigwa na kuongeza:

“Aliyoyasema tangu siku ya kwanza alipoingia madarakani ndiyo anayoyatekeleza na sisi lazima tutekeleze maelekezo yake kuhakikisha kuna uhuru wa vyombo vya habari, kuhakikisha waandishi wa Habari hawabughudhiwi lakini kuendelea kujenga mazingira bora kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao,”.

Kongamano hilo la Maadhimisho ya Siku ya Siku ya Uhuru wa Habari linatarajiwa kufungwa leo Aprili 29, 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

spot_img

Latest articles

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa...

Vunjabei, Sara kuisaka heshima ya Tanzania One ulingoni

Na Winfrida Mtoi MABONDIA wa ngumi za kulipwa, Halima Ramadhani maarufu Vunjabei na Sara Alex...

More like this

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa...