Majaliwa: Kuundwa kwa JAB ni hatua ya kuimarisha na kuboresha sekta ya Habari

Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua kadhaa katika kuimarisha na kuboresha sekta ya habari nchini ikiwa ni pamoja na kuunda Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari.

Waziri Mkuu amesema hayo leo Aprili 29, 2025 wakati akifunga Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Arusha kwa siku mbili.

“Kwenye sekta ya habari na utangazaji, falsafa ya “4Rs” za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alizozibainisha baada ya kuingia madarakani mwezi Machi 2021, imetekelezwa kwa vitendo hususani kwenye eneo la “Reforms” (Mageuzi),” amesema Waziri Mkuu na kuongeza:

“Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza falsafa hii imechukuwa hatua mbalimbali kuimarisha sekta ya habari na utangazaji nchini kwa kuunda chombo kipya cha kushughulikia usajili wa taaluma ya waandishi wa habari yaani Bodi ya Ithibati,”.

Majaliwa amesema Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari iliyozinduliwa mwaka huu ina jukumu la kusimamia viwango vya kitaaluma kwa wanahabari ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa matakwa ya kisheria chini ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.

Amesema hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni kuhakikisha inawezesha shirika la Habari la utangazaji kuwepo kisheria pamoja na kuimarisha Idara ya Habari Maelezo kwa kununua vitendea kazi vikiwemo Magari na vifaa vya kurushia matangazo mbashara.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu inayosema ‘Uhabarishaji kwenye Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba katika uhuru wa vyombo vya habari’ inalenga kujadili athari za teknolojia ya akili mnemba katika uendeshaji wa vyombo vya Habari na uhuru wake.

Amesema Serikali katika kuhakikisha Akili Mnemba (AI) inatumika kwa njia inayowezesha badala ya kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari, imeanzisha mchakato wa kuandaa sera maalum ya AI na waandishi wanaowajibu wa kuchangia ili kupata sera nzuri.

“Sera hii itatoa mwongozo wa matumizi ya AI katika vyombo vya habari, ili kuhakikisha kwamba teknolojia mpya zinaendana na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari, uwazi, na uadilifu wa uandishi wa Habari, hivyo mtumie muda wenu hapa kujadili na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera hiyo,” amesema Majaliwa.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...