Kamati Tendaji ya Mradi wa SOFF yakutana kutathmini utekelezaji wa mpango kazi uliyoidhinishwa

Na Mwandishi Wetu

KAMATI Tendaji ya Utekelezaji wa Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa (SOFF) imekutana mkoani Morogoro ambapo moja ya masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na kutathimini utekelezaji wa mpango kazi wa mwaka 2024, kupokea na kupitsha mpango kazi na bajeti kwa mwaka 2025.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a, wakati akifungua rasmi mkutano wa pili wa kamati hiyo katika Ukumbi wa hoteli ya Cate, Morogoro.

Dkt. Chang’a ameishukuru Kamati hiyo pamoja na Sekretarieti kwa kazi kubwa iliyofanyika katika kuhakikisha majukumu ya mradi kwa mwaka 2024 yanatekelezwa kwa ufanisi ikiwemo hafla ya uzinduzi wa mradi huo.

Dkt. Chang’a alifafanua TMA iliandaa mpango kazi wa utekelezaji wa maelekezo matano yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa Uzinduzi yakiwemo masuala ya utekelezaji wa shughuli za mradi kwa wakati na ufanisi pamoja na ushirikiano baina wa wadau wa Mradi.

Awali wakati wa ufunguzi, Naibu Mwakilishi Mkazi Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amos Manyama amesisitiza kuwa UNDP itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania, TMA na Wadau wengine wa mradi kuhakikisha malengo ya SOFF yanafikiwa.

Aidha ameendelea kusisitiza haja ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na TMA katika kuimarisha huduma za haki ya hewa hata baada ya mradi.

Katika hatua nyingine, Kamati ilipokea na kuidhinisha Mpango Kazi wa mwaka 2025, taarifa ya hesabu kwa mwaka 2024 na Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mradi.

SOFF ni Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa kwa Nchi zinazoendelea na Nchi za Visiwa vidogo.

Lengo la Mradi ni kuimarisha huduma za hali ya hewa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi ili kulinda maisha ya watu na mali ikiwemo kuboresha zaidi miundombinu ya uangazi wa hali ya hewa na kuhakikisha Tanzania inakidhi mahitaji ya wadau wa Kitaifa na Kimataifa.

Mradi huu unatekelezwa kwa muda wa miaka minne kuanzia Julai 2024 hadi Disemba 2027.

spot_img

Latest articles

Wanawake TRA Wapongezwa kwa Mchango wa Ukusanyaji Mapato

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, amewapongeza wanawake wa...

Mchungaji Kimaro: Miradi ya Familia Ndio Suluhisho la Ajira kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu  MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjiri Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama Dk....

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani: TRA Yakabidhi Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Milioni 40

Na Tatu Mohamed KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8,...

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

More like this

Wanawake TRA Wapongezwa kwa Mchango wa Ukusanyaji Mapato

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, amewapongeza wanawake wa...

Mchungaji Kimaro: Miradi ya Familia Ndio Suluhisho la Ajira kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu  MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjiri Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama Dk....

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani: TRA Yakabidhi Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Milioni 40

Na Tatu Mohamed KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8,...