Kapinga: Vitongoji 9000 kusambaziwa umeme mwaka 2025/26

📌 Majimbo yaendelea kufaidika na mradi wa umeme wa Vitongoji 15

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imekamilisha kazi ya kupeleka umeme kwenye Vijiji vyote Tanzania Bara na nguvu sasa inaelekezwa kwenye vitongoji.

Kapinga ameeleza kuwa, pamoja na kazi ya kupeleka umeme vitongojini inayoendelea sasa, Serikali ina mkakati wa kupeleka umeme kwenye Vitongoji 9,000 katika mwaka ujao wa fedha wa 2025/26.

Ameeleza hayo leo Aprili 09, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Nkansi Kusini, Vicent Mbogo aliyeuliza ni lini Serikali itapeleka umeme katika Vitongoji vilivyopo Jimbo la Nkansi Kusini.

“Kitongoji cha Lupata kilichopo Kata ya Kizumbi kitapata umeme kupitia mradi wa Vitongoji 15 vya kila Mbunge, na kitongoji cha Lwela Kata ya Mpembe kitapata umeme kupitia miradi itakayokuja,” amesema Kapinga.

Akijibu swali Mbunge wa Momba, Condester Sichwale aliyeuliza ni upi mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme kwenye Vitongoji vya Tarafa za Ndarambu, Msangano na Kamsambu, Kapinga amesema Serikali inao mkakati wa kutekeleza miradi ya umeme kwenye Vitongoji na hivi sasa inatekeleza mradi wa kupeleka umeme kwenye Vitongoji 15 kwa kila Jimbo.

Ameongeza kuwa katika miradi wa Vitongoji 15 wakandarasi wamemaliza kazi za awali na sasa hivi wapo katika hatua ya kupata vifaa.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...