Tanesco yashinda tena Tuzo za Ubora Huduma kwa Wateja za CICM

📌Urahisi wa upatikanaji whuduma kwa njia za kidigitali watajwa moja ya kigezo cha kushinda tuzo hiyo

📌MD Gissima aibuka kidedea kwa Kusimamia Maboresho yenye tija huduma kwa wateja Sekta ya Umma.

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) kwa mara nyingine tena limeshinda tuzo ya the ”Most improved Organization” eneo la huduma kwa wateja iliyotolewa na Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management(CICM).

Tuzo hizo zimetolewa 28, Machi 2025 jijini Dar es Salaam ambapo Shirika limepata tuzo hiyo baada ya kufanya maboresho ya kutumia njia za kidigitali kurahisisha mchakato wa maombi ya umeme na upatikanaji wa huduma kuwa mwepesi kwa wateja wake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO , Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Irene Gowelle amesema Tuzo hizo ni heshima kwa Shirika ikiwa ni ishara nzuri ya maboresho yanayofanyika kutambuliwa na kuthaminiwa.

“Tuzo hizi ni heshima kubwa kwa TANESCO, zinatuongezea ari ya kufanya vizuri zaidi,tutaongeza ubunifu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wetu,’’.

Aidha , Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Gissima Nyamo-Hanga na yeye alishinda Tuzo ya heshima ya Kiongozi anayefanya mabadiliko chanya yenye tija upande wa huduma kwa wateja katika Sekta ya Umma.

Tuzo za Tanzania Service excellence awards hutolewa kila mwaka na zinalenga kutambua Taasisi za Umma na binafsi zinazoimarisha na kuboresha huduma bora kwa wateja wake.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this